Habari Za Un

14 APRILI 2026

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Waziri wa sheria na ambaye pia ni mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Dkt. Emmanuel Ugirashebuja amezungumza na Idhaa hii na anaeleza siri ya wananchi wa Rwanda kuweza kuishi kwa amani baada ya mauaji hayo.Kama mapigano yataendelea nchini Sudan hadi mwaka 2030, umaskini wa kupindukia unaweza kuongezeka na kuvuka asilimia 60, huku watu wengine milioni 34 wakitumbukia kwenye ufukara, imesema Ripoti ya uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) iliyotolewa leo Sudan na Marekani ikiwa kesho inatimia miaka mitatu kamili tangu kuanza kwa vita.Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa kauli zao tofauti tofauti kuhusu miaka mitatu ya vita nchini Sudan ambapo lile la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto wanaendelea kulipa gharama ya vita kwani zaidi ya watoto 245 wameuawa au kujeruhiwa nchini humo tangu Januari hadi Machi mwaka huu, huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani au droni yamesababi