Synopsis
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Episodes
-
Je dunia iko katika njia sahihi kutimiza lengo la kumaliza njaa kufikia 2030?
26/05/2025 Duration: 09minJumatano ya Mei 28 2025, dunia itaadhimisha siku ya njaa ulimwenguni, siku hii ikilenga kutoa hamasa na kuchochea hatua kuchukuliwa ili kumaliza njaa duniani. Kulingana na ripoti ya kimtaifa ya 2025 kuhusu migogoro ya Chakula, zaidi ya watu milioni 295.3 katika nchi 53 wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula.
-
Uchakataji wa plastiki katika kuhifadhi mazingira ya bahari na kupata mapato
15/05/2025 Duration: 09minJamii za Pwani ya Kenya, zimekumbatia uchakataji wa plastiki kukabili tatizo la uchafuzi utokanao na taka za plastiki ambapo mujibu wa shirika la mazingira la UNEP, kila siku, kiasi sawa cha malori 2,000 ya kuzoa taka yaliyojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito, na maziwa ya ulimwengu.
-
Mabadiliko ya tabianchi: Hali ya mifumo ya sheria katika kushughulikia ukatili wa kijinsia.
05/05/2025 Duration: 10min -
Mabadiliko ya tabianchi yachochea ongezeko la ukatili wa kijinsia
28/04/2025 Duration: 10minRipoti hiyo mpya ya UN Spotlight initiative, imebaini kuwa mabadiliko yatabianchi yameendelea kuzidisha mogogoro ya kijamii na kiuchumi ambayo inachochea kuongezeka kwa viwango vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana.