Synopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodes
-
Utayari wa ukanda wa Afrika kupambana na magonjwa ya milipuko
19/02/2025 Duration: 10minKatika siku za hivi punde magonjwa ya milipuko imeripotiwa katika mataifa ya Afrika ,ikiwemo Ebola Marburg na Mpox
-
Juhudi za Guinea kumaliza ugonjwa wa Malale mojawapo ya magonjwa yaliyotengwa
05/02/2025 Duration: 10minGuinea itakuwa ni taifa la nane la Afrika kuthibitishwa kuangamiza ugonjwa wa malale Guinea imekuwa ilishiriki katika majaribio ya matibabu ya ugonjwa wa malale ambayo yalifanyiwa utafiti mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoTimu ya madaktari kutoka DRC na Guinea walishirikishwa kwenye majaribio hayo na kwenye makala haya tumezungumza na Dkt Chirac Bulanga kutoka DRC
-
Ugonjwa wa Ukoma bado ni changamoto kubwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
29/01/2025 Duration: 09minDRC imeripoti maambukizi ya Ukoma mwisho wa mwaka jana na pia mwaka huu Ukoma ni ugonjwa unaoathiri sana ngozi na unaweza kuharibu baadhi ya viungo kama vile mikono ,miguu na hufanya mtu kutengwa na jamii
-
Ongezeko la mafua na magonjwa yenye dalili za mafua wakati wa joto
21/01/2025 Duration: 09minKumeendelea kushuhudiwa kwa idadi kubwa ya watu wanaougua mafua au magonjwa yanayoathiri mfumu wa kupumua mwezi Januari ambao una joto jingi na vumbi. Hii inajiri wakati China ikiwa imeripoti mlipuko wa ugonjwa wa Human metapneumovirus ,HPMV unaofanana na COVID 19 .Daktari Juma Maleve kutoka Hospitali ya rufaa ya Mombasa ,Pwani ya Kenya anafafanua.