Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:02:42
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Episodes

  • Muungano wa Rais wa Kenya W. Ruto na Raila Odinga, hali mbaya ya kibinadamu DRC

    08/03/2025 Duration: 20min

    Rais wa Kenya William Ruto na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wameungana kisiasa rasmi, hali ya mzozo wa mashariki mwa DRC Kuchukua sura mpya, vikwazo vya kiuchumi kuikumba nchi ya Rwanda kufuatia uungwaji mkono wake kwa kundi la waasi la M23, Kiongozi wa kijeshi wa Gabon jenerali Oligui Nguema kuwania urais mwezi ujao, mzozo wa kibiashara kati ya Marekani nchi mataifa kadhaa, lakini pia mzozo wa Ukraine na Urusi.

  • Rais Donald Trump na Volodymyr Zelensky watofautiana kuhusu vita nchini Ukraine

    04/03/2025 Duration: 19min

    Wiki hii kwenye habari za ulimwengu tunaangalia majibizano makali kati ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika Ikulu ya White House, pia tunaangalia mikakati inayowekwa kumaliza mgogoro wa DRC huku Rwanda ikisema haitishwi kutengwa na ulimwengu, Somalia na Ethiopia zarejesha uhusiano wa kidiplomasia, mkutano wa G20 ukikamilika kule Afrika Kusini bila mwafaka kufikiwa.

  • Kizza Besigye wa Uganda ashtakiwa kwa uhaini, Kenya na Sudan zatofautiana kuhusu RSF

    23/02/2025 Duration: 19min

    Habari za wiki hii ni pamoja na hali kule nchini Mashariki mwa DRC, utata wa kidplomasia uanozingira Kenya na Sudan, tutaangazia pia kesi ya kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, lakini tutaangalia kipindi cha mpito nchini Niger. Tumedadisi pia hali kufikia sasa ya vita vya kule Gaza na misimamo ya viongozi mbalimbali wa ulimwengu.

  • Mkutano wa AU kuhusu mzozo wa DRC, waasi wa M23 waudhibiti mji wa Bukavu

    15/02/2025 Duration: 20min

    Makala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia ambapo wamemchagua kiongozi wa tume ya Umoja wa Afrika AU kati ya wagombea watatu, lakini pia mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda dhidi ya jeshi la serikali FARDC na ambao sasa wameudhibiti mji wa Bukavu huko Kivu kusini mashariki mwa DRC, mapigano ya nchini Sudan, siasa za Uganda na pia kwenye nchi za Afrika Magharibi. Lakini pia zoezi la ubadirishanaji wa mateka huko Gaza

page 2 from 2